TUJIKUMBUSHE

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo ni heri mama wee

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania, ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu hakika

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania, watu wengi wanakusifu,
Siasa yako na desturi, ilituletea uhuru
Hatuwezi kusahau sisi, mambo mema ya kwetu hakika

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania, Kaaribu wasio kwao,
Wenye shida na taabu, hukimbizwa na walowezi

Tanzania yawakaribisha, mpigane kiume chema wee

Tanzania Tanzania, heri yako kwa mataifa

Tanzania Tanzania, watu wako ni wema sana
Nchi nyingi zakuota, nuru yako hakuna tena
Na wageni wakukimbilia, ngome yako imara kweli wee

Tanzania Tanzania, Mola awe nawe daima

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

Love podcasts or audiobooks? Learn on the go with our new app.