SIO DHAMBI SIO UDHAIFU

Nilipokua mdogo Mlezi wangu aliniambia mara kwa mara mtoto wa kiume halii,hata pale niipoumizwa dhahiri aliniambia vumilia jikaze,wewe mtoto wa kiume..kiukweli maneno yale yalijenga msingi moyoni mwangu,nikawa mtu wa kutabasamu kila mara,kila siku.huzuni yangu haikuonekana machoni,nililia mwenyewe moyoni.kumbe nilijaza sumu ya ukatili na uchungu mwingi moyoni.nikawa muovu,muuaji na mzimisha furaha za wengi kwa tabasamu langu maana niliwafunza wengine pia kuvumilia hata pale kisu kilipokua shingoni mwao..
siku moja rafiki yangu mmoja alifukuzwa kazi wakati umebaki mwezi mmoja alipe kodi ya nyumba na kumalizia ada yake ya chuo. mshahara wake ulikua laki 6 na 80 akipiga na vi overtime inagonga mpaka nane au tisa ,hesabu zake zilikua alipe ada laki nne nyingine alikua analipiwa na bodi,kisha alipe kodi miezi mitatu( laki 3) yalipotokea haya alikuaja kwangu kunieleza na majibu yangu yakawa yale yale USILIE,USIHUZUNIKE wewe mtoto wa kiume pambana.lakini mwezi ulikatika pasipo yeye kupata hela wala mimi akashindwa kufanya mitihani yake na chumba akafukuzwa na kuahamia kwangu,miezi miwili mbele nilifiwa na mtu wangu wa karibu,wakati napokea taarifa hizi nilikua pamoja na yeye akaniambia maneno yale yale niliokuwa nikiwaambia.niliumia sana moyoni ila ikanibidi nijikaze mbele yake huku kifua kimejaa maumivu, ndio yule swahiba wangu akaniambia acha ujinga huo,wewe ushakua sasa,wajua nini maana ya maumivu ya moyo,usiyazuie,lia tu,lia tena kwa sauti,machozi yatoke na uchungu uishe.niifanya hivyo siku nzima na baada yahapo moyo ulijaa Amani,nikawaza mapya vyema na yenye heri ikiwemo kumuombea marehemu.tangu siku hiyo #Nimejifunza UJASIRI sio kukaa na uchungu moyoni ni kutatua lililo moyoni na kusonga mbele.kulia sio dhambi sio udhaifu.

#Fikrazajamii #hatuazamtoano #hekayazamtaa

--

--

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

Love podcasts or audiobooks? Learn on the go with our new app.

Get the Medium app

A button that says 'Download on the App Store', and if clicked it will lead you to the iOS App store
A button that says 'Get it on, Google Play', and if clicked it will lead you to the Google Play store