OPEN LETTER TO MY FELLOW

Mimi niko poa kabisa.Ila dunia haijaisha uchungu.na ingawa am lucky to have u on my side and my family too still dunia ni chungu kwangu.

Labda sijajua dhumuni langu katika hii dunia,ndio maana muumba akanipa wewe lakini nimeshindwa kujua ww ni nani !?
natafakari makasirikio ya hii dunia dhidi yangu,bado sijioni ni mkosefu wa kustahili hii adhabu.ni kweli sijui kosa langu,na wala sijui kwanini unataka unifunze adabu.
je ni kosa kuipenda dunia yangu!? je ni kosa kuiamini akili yangu !? ama kosa ni kukuweka pembeni yangu.!?

Naamini Mama & baba ni miungu ya pili ya hii dunia,right! Na wananipenda sana mtoto wao wa kumzaa,na wamenipa kibali na baraka kwa kunifunza yaliyomo,na kwa umakini sana nimelielewa somo.ila mbona bado dunia ni chungu,je kuna lililonyuma ya walimwengu.!? silijui hatulijui ndio maana umeshindwa kunisaidia kuvuka hili daraja la uchungu.basi sitokosea kusema wewe haukuwa chaguo sahihi,kitabu chako ni funzo ambalo halina zangu wajihi.ndio maana dunia kwangu bado ni chungu.

lakini mbona ni wewe rafiki yangu uliyebeba haya maono yangu.ukanisogeza hatua tatu toka mtaani kwangu.
ukanifunza kuishi hivi,ukanifunza imani hii,na zaidi ukanikabidhi kwenye mikono salama ya sala.asubuhi mchana na usiku napolala.
wapi nimekosea!? wapi tumekosea !? mpaka tuendelee kuonja uchungu.Wakati dunia haikuumbwa na uchungu..

Dah afadhali sasa nimekumbuka,ulinifunza maisha yangu,ndio safari yangu,nisikate tamaa kamwe dhidi maisha yangu, huu uchungu ndio somo kuu la maisha yangu.

TUVUMILIANE TUPENDANE RAFIKI YANGU.
WEWE NDIO MIMI.

Ila Ndugu yangu wewe wajua fika mimi ni dhaifu mbele yako,ila mimi ndio kinga yako kuu.
Japo hakuna mkamilifu wote tuna mapungufu,kila lisilo jema kwangu basi litaathiri kwako pia.na kila fanikio langu basi ni sherehe yako pia.
ila ni kwanini kwanini kila kitu ni wewe,na kila siku ni wewe.
anayenistiri ni wewe na anaye nisaliti ni wewe.
Jana dunia ilikua chungu sababu ya wewe.na leo faraja inatoka kwako.lakini ndoto yangu kesho wewe waijua.na ulifurahi sana siku ulipoijua.
furaha yako haikuishia kunipongeza tu ila ulinishauri mengi sana na nilifarijika sana.na leo tuko pamoja safirini.japo dunia ni chungu,nusu ya uchungu unaonikabiri nawe waujua.ndio maana NAKUPENDA RAFIKI YANGU.imebidi tu nikuandikie barua ya wazi rafiki,ila pia wajue najua wewe una unafiki,mnafiki niliyekuchagua kuwa rafiki wa milele.na waliache letu pendo hata kama lina chungu tele.
#Hatuazamtoano #fikrazajamii #rafiki_ana_rafiki_pia

Note: Picha haihusiani na maelezo

--

--

--

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

Get the Medium app

A button that says 'Download on the App Store', and if clicked it will lead you to the iOS App store
A button that says 'Get it on, Google Play', and if clicked it will lead you to the Google Play store
Dr.John Heshima

Dr.John Heshima

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

More from Medium

Love Does not Conquer All

El vacio (emptiness)

A lake with tree branches over its banks.

DID YOU KNOW ?