NITARUDIA TENA NA LEO.

Mara ya kwanza kabisa hakuna aliyetaka kuamini Kama ni kweli inawezekana.japo mifano mingi ilitolewa lakini haikuwaingia akilini kabisa.

Mmoja wa maswahiba wa bwana yule akasema kamwe yeye hawezi kutoka kibali Cha kuruhusu ndugu yake anyanyasike,maana yeye aliona ile hali ni manyanyaso tu,aliona kuwa ni wzo kubwa Sana kwa ndugu yule kulitekeleza.alizidi kwenda mbali zaidi kwakumtaka ndugu yake huyo ambaye anamuona akinyanyasika kimawazo achague moja Kati mafungu mawili aliyoyatenga mezani.

Ila kwakuwa beans yule alikua na dhamira hiyo ya dhati naye hakutaka kuyumbishwa hata kidogo na jamii yake ile iliomzunguka.na hata alipotakwa achague fungu moja,bila kusita alichagua fungu lile lile aliolileta mezani.
Haukua uamuzi mzuri kwa wafanya biashara wazoefu ndio maana ndugu zake wengine hawakukabaliana naye,wakamuacha apambane mwenyewe.
Dhamira yake ilisimama imara na chagizo lililo moyoni mwake,kwakweli aliipenda Sana biashara hii na wazo hili alilielewa Sana,hivyo hakutaka hata wasaa wakuliacha lipite.

Na bahati nzuri wazo hili nalo lilijitabanahisha na kujimilikisha Nafsi ya bwana yule baraabara.kitu kilichomtia faraja bwana yule,na jambo liliompa hamasa bwana yule na hata pale kulipotokea biashara kuyumba na wazo kutaka kuhamishwa ndani ya utendaji wake.bwana yule alikubali kuwa mtu wa kujifunza akiamini kuwa limeshindikana leo bali sio milele hivyo kesho atarudia tena.
Ikiwa siku,miezi na sasa zaidi ya miaka wazo lile Bado linaishi ndani ya jamaa yule,limekua likistawihi,kunawiri na hata kuyumba na kusinyaa pia.bado bwana yule hajakata tamaa na umiliki na uendeshaji wa hili wazo,anaendelea kulipigania,kulitenda kila uchao na mara zote Asubuhi akiamka husisitiza NITARUDI TENA NA LEO...

UWE NA SIKU NJEMA NA WIKI NJEMA..

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST