KWAHERI RAIS MAGUFULI “MIAKA SITA YA KISHUJAA SANA”

Maandiko yanasema kila nafsi itaonja umauti na sisi tu mavumbi na mavumbini tutarejea.hii inamaanisha ya kwamba hapa duniani si makazi ya nafsi zetu ya kudumu,tunapita tu na huu mwili ni mavumbi tu.

Usiku wa tarehe 17 March 2021 umekua mrefu zaidi kwa Watanzania kuliko usiku mwingine wowote ule tangu kuzaliwa kwa taifa hili.

Kwa Mara ya kwanza tumeondokewa na kiongozi mkuu wa nchi,jemedari na mzazi wa taifa anbaye bado hakuwa amemaliza muda wake.Rais John Pombe Joseph Magufuli ameaga duniani wakati akiwa bado ni Amri jeshi mkuu wa nchi.

Ni mengi Sana yapo ya kumueleza Mwamba,Jiwe,Jabali la watanzania kwa miaka 61 aliopata kuishi katika hii dunia.yenye historia ndefu ya kuvutia,kuhamasisha na kujenga pia,Ila leo nitazungumzia tu “MIAKA SITA YA UTAWALA WAKE WA KISHUJAA KATIKA TAIFA HILI TEULE”

ULIKUA NI UTAWALA WENYE UONGOZI NA UTHUBUTU

katika kitu kikubwa ambacho Rais Magufuli umetuachia na tutakukumbuka siku zote na milele yote ni hili la uongozi wenye uthubutu.

Siku zote za utawala wako umekua mthubutu wa kutenda na kufikiri Yale ambayo wengi hatuwaza.hukuogopa kujaribu kila Jambo jema uliliona Lina manufaa kwa taifa na watanzania wanyonge.

Hukuogopa kuchukiwa na wachache kwa maslahi ya wengi,ndio maana ulithubutu kwenye upanuzi wa njia nane za kimara Hadi kibaha,Leo watanzania tunateleza tu,lakini pamoja jumuia zote za kimataifa na wanaharakati kukupinga,bado ulithubutu ujenzi wa bwawa la mwalimu nyerere ambalo litatutoa kabisa Tanzania kwenye uhaba wa nishati ya umeme.

Wakati dunia ikiamini biashara ya usafiri wa anga,ni biashara ambayo serikali haipaswi kuwekeza kwa asilimia 100,wewe ulithubutu kuifanya kwa utofauti na Sasa taifa linajivunia kuwa na shirika la anga hai lenye ndege zake

Uthubutu wako kiutendaji haukuwa tu kwenye miradi ya maendeleo lakini pia kwenye usimamizi wa Mali na Hali za watanzania..wengi walikushangaa Sana ulipoamua kuunda tume ya Makinikia ,na kujenga ukuta mererani Ila Leo ndio sisi ndio mashahidi wa utajiri unatokana na madini yetu.

Tabia hii haikuishia kwake tu ,walifundisha na kuwarithisha viongozi wote waliokuwa chini yake,tuliona mawaziri,wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi wa halmashauri pia,wakijawa na uthubutu mkubwa katika kuwatumikia wananchi hasahasa wale wanyonge

UMETUACHIA UJASIRI na KUJIAMINI.SASA NI TAIFA IMARA

Ikiwa ni miaka mingi tumeishi katika fikra za kuamini sisi ni taifa maskini na tegemezi.wewe ukiona tofauti Sana na sisi na ukatujengea ujasiri wa kuamini nguvu yetu.

Ndani ya miaka yako yote sita ya utawala, asilimia 75 ya miradi mikubwa uliotekeleza ulitumia fedha zetu za ndani,ulitumia Kodi zetu vizuri na ukatujenga nasi katika fikra za ujasiri huo.

Lakini si tu miradi hata maamuzi yako kiutendaji yalijaa ujasiri na kujiamini na watanzania umetufunzà Hilo sasa.hukuogopa vitisho vya mataifa makubwa kuhusu muundo wa utendaji wa serikali yako,na Chama chako.uliamini mabadiriko uliyokuwa unatujengea na kweli yalifanya kazi..kwani sisi sote ni mashahidi wahili, jinsi ulivyotengeneza ujasiri kwa wengi vijana ndani uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya Chama najinsi ulivyonyenyua viongozi wapya na walio chaguo la kweli la wanachama.ikawa ndio mwisho wa zile zama za wenye fedha na matajiri kuendesha mambo wanavyotaka.na tabia ya wachache kujihalalisha utukufu na mamlaka imeisha ndani miaka sita ya utawala wako.

SAUTI YA WANYONGE,MASKINI NA WANANCHI WA HALI YA CHINI ILISIKIKA.

Tanzania ya Magufuli ilikua Tanzania ya usawa,serikali iliowajibika kwaajili ya wale wote wasio kuwa na sehemu ya kupaza sauti yao.utawala wake ulijapambanua wazi Kama utawala wa watanzania maskini na wanyonge,na kamwe haikua na kificho katika Hilo.

Wale wote waliozoea kuishi kwa mabavu na ubabe kwa raia wanyonge walikiona kimtema kuni.waliwajibishwa ipasavyo.

Nimengi mno ambayo ameyatenda kwa wanyonge wa taifa hili Ila kwa machache tujikumbushe haya

· Vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo – kila mfanyabiashara alipaswa kulipia kiasi Cha Tz 20000 na kupewa kitambulisho kilichomuwezesha kufanya biashara popote ndani ya jiji la Dar es salaam

· Mikopo ya halmashauri kwa wajasiriamali (hasa kina mama na vijana )…ambapo kila wilaya ilipaswa kutoa asilimia 10ya mapato yake yote kwenda kwakina mama ,walemavu na vijana..mikopo ya vikundi isiyo kuwa na riba kabisa.

· Uboreshaji wa huduma za afya vijijini..Mh aliona Hali halisi ya kina mama wanyonge wa vijijini wanavyotaabika kupata huduma za afya,hasa afya ya uzazi.hivyo ndani ya miaka yake sita chini ya waziri wa Tamisem,vituo vya afya zaidi ya elfu moja(1000) viimejengwa ,huduma za dawa hospital ziliboreshwa na upatikanaji wake pia,alipandisha na bajeti ya wizara ya afya Mara tatu ya aliyoikuta.

· Aliboresha mikopo ya wasomi vyuo vikuu na kutoa elimu bure (shule ya msingi mpaka kidato Cha 12)

· Aliondoa gharama za huduma kwenye nishati ya umeme (service charge)

Wakati wa ziara zake za kikazi alikua ni mwepesi wa kusikiliza hoja na malalamiko ya wanyonge na kuyatatua papo kwa hapo.hakua mtu wa kusubiri michakato kwenye kufanya maamuzi na Jambo lenye maslahi na wanyonge.

USALAMA WA TANZANIA NA MALI ZETU ULIONGEZEKA

Huko nyuma ilikua kawaida kusikia milio risasi na mabomu kilawiki,matukio uvunjaji,unyang'aji Mali za watu yalikua matukio ya kila siku,kila wiki.

Lakini ndani ya miaka yako sita ya utawala,uliboresha Sana jeshi la ulinzi na jeshi la polisi pia.na ukatoa msimamo wako wa wazi kwa watendaji wake.hali hii ilipelekea kusafisha kabisa jiji na Miji na kutufanya wananchi tuishi kwa Amani zaidi.

Ule mchezo wa uvamizi wa benki na vituo vya mafuta umeisha kabisa Tanzania.hata ule mtindo wa uvamizi wa maduka makubwa mchana kweupe hadharani kabisa umekata.hakika umeniacha nchi ikiwa salama,Tanzania ni salama Sasa.

HAKUNA MWENYE PRESHA NA ULAYA TENA BABA,UMETUJENGEA UZALENDO.

Kabla ya utawala wako Hayati John Pombe Magufuli,watanzania walio wengi hawakuwa na uthubutu wa kusimama kutetea taifa la Tanzania,lakini Wala hatukujali Jambo lolote linalohusu nchi yetu na taifa jingine..hatukuona kwetu Kama mahali pakukimbilia,sababu tu hatukua na uhakika wa maendeleo ya taifa hili…uzalendo wetu ulipungua Sana.

Kwa umahiri wako mkubwa wa usimamizi wa miradi ya maendeleo,uwazi na maono yako katika maendeleo.yamebadiri taswira ya nchi hii,yamebadiri mawazo na utashi wa watanzania wengi.

Ulikua jasiri katika kusimamia utanzania na uhalali wa kuwa mtanzania.napale palipo na kikwazo Basi uliondoa na kuboresha Jambo ambalo kila mmoja wetu angejivunia..

Ndio maana umeboresha Sana sekta ya afya,na hospital zetu kubwa za rufaa kuaminika,lakini umeboresha miundo mbinu ya Barabara,reli ,na meli kiasi kwamba hakuna Shaka na usafiri wa ndani,umeenganisha mtandao wa Barabara nchi nzima na kuboresha usafiri wa anga.

Hata UMEME suala lililo kuwa Kero kubwa ya uwekezaji Tanzania na maendeleo ya watanzania nalo limekwisha.mgawo wa ajabu ajabu uliokuwepo hapo nyuma Sasa tumesahau.

Watanzania Sasa tunajivunia nchi yetu,maendeleo yetu na tunaona fahari kusema Mimi ni “Mtanzania”

Umetuheshimisha duniani kwenye suala la korona,ukatuheshimisha kwa mabeberu kwa kuvunja mirija ya ukandamizaji kwenye mikatba ya madini..

ASANTE MAGUFULI,KWA MIAKA SITA YA USHUJAA NA KUACHA ALAMA YA KUDUMU MILELE

Imeandaliwa na Dr.John Heshima

--

--

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

Love podcasts or audiobooks? Learn on the go with our new app.

Get the Medium app

A button that says 'Download on the App Store', and if clicked it will lead you to the iOS App store
A button that says 'Get it on, Google Play', and if clicked it will lead you to the Google Play store
Dr.John Heshima

Dr.John Heshima

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

More from Medium

𝐑𝐄𝐒𝐓 𝐅𝐎𝐑 𝐏𝐑𝐎𝐃𝐔𝐂𝐓𝐈𝐕𝐈𝐓𝐘 or one-day mega vacation

Entries into the lighthouse project now live on Moonscape November 20, 2021 by Joshua Asuquo Nya

How to Survive Technological Disruption

Watermelon in Easter Hay