HIVI NI KWELI !?

Ni swali jepesi lenye jibu la ndio au hapana,lakini kabla hujajibu linahitaji tafiti isiyo rasmi kujihakiki.

Iko hivi,bi mkubwa,mamaake mwenyewe yupo mjini baada ya kaziara kafupi ka kuwatembelea marafiki zake wa zamani miji kadhaa ya kusini mpaka kaskazini mwa Tanzania(kama mgombea vile 😂)
Wakati tumekaa tukipiga stori jinsi alivyoona mabadiliko ya nchi,maana kuna miji imepita miaka 20 tangu alipoenda mara ya mwisho.tbc wakawa wanaonyesha nyomi la kampeni za @tunduantiphaslissu akiwa mbarali
Nikamsikia akisema "NINGETAMANI APITE KASULU NIKIWA NIMERUDI,NAMI NIKAMUONE"
basi nami nikamjibu kimasikhara tu "tuombe uzima utamuona tu mama yangu,bado kuna miji mingi mnaweza kukutana huko"
Baada ya kumjibu hivyo huku tbc wakamuonesha rais Magufuli akimvisha kofia mwanamuziki @officialalikiba__ akaniuliza ile kofia ni yanini!? Nikamjibu ni zawadi ya heshima na sio yeye wakwanza alishamvisha @diamondplatnumz na @harmonize_tz akauliza tena mbona mikutano ya @chadematzofficial sioni wasanii!? Nikamjibu hawana na nyomi wanakusanya,na hapo hapo nikamuuliza "mama unampenda Sana lissu" jibu lake ndio lilonifanya nijiulize HIVI NI KWELI!? nikaona sio mbaya nikawauliza na ndugu zangu hapa
HIVI NI KWELI !?
Mama Alinijibu hivi "SIO KWAMBA NAIPENDA CHADEMA WALA LISSU,NAMPENDA SANA MAGUFULI ILA NATAKA KUMUONA LISSU MAANA SI MFAHAMU NA NIKASHANGAE MIUJIZA YA MUNGU...

Love podcasts or audiobooks? Learn on the go with our new app.