STORI YA KIJAZI.

Ni mzaliwa wa mkuranga,pwani.mtoto wa pekee wa bi rehema,marehemu baba yake mzee Hamis alikua mvuvi wa samaki katika bahari hindi.na ndio ujuzi pekee aliomrithisha mwanae kijazi.
Kijazi hakupata nafasi ya kuendelea na shule alipohitimu elimu yake ya msingi,sababu mama hakua na uwezo tu wakumnunulia sare za shule.
Hivyo akawa mara nyingi akijumuika na na wavuvi wengine kwenda kuvua na kisha kuwanadi samaki waliopata ufukweni na mara Chache Sana alizungusha Hadi mitaani.kwa ufupi yeye ndio alikua baba wa familia.
Alipenda Sana kuchezea maji,hivyo muda mwingi wa jioni utamkuta baharini akiogelea,mara Chache Sana ungemkuta yupo na wenzie,alipenda kuoga peke yake.
Na Hakua na marafiki wengi sababu rika lake wengi wao walikua wakiendelea na masomo ya sekondari.
Siku moja wakiwa baharini na wavuvi wenzie wanatafuta riziki,kwa mbali kama mita Mia tano waliona chombo(boat ya mashine) ikija kwa kasi Sana upande wao.walishtuka na kuogopa Sana hivyo walitoa nanga ya upesi Sana na kuanza kupiga makasia kuelekea upande mwingine.bahati mbaya ilikua upande wao ile boati iliwafikia na kuwaparamia na kupinduka.kwa kua ile boat ilikua kwa kasi ilipowagonga iliwarusha mbali na mtumbwi wao huku nayo ikipinduka mazingira hayo hayo.
Kijazi ndio alikua wakwanza kuibuka toka majini..hakuona mtu yoyote Yule akiogelea haraka Hadi ulipoangukia mtumbwi wao na kuugeuza ,ulitoboka kidogo ukawa unaingiza maji kidogo...alikaa pale juu kwa dakika kadhaa pasipo kuona mtu

Alipiga moyo konde kisha aliingia kwenye maji na kuanza kumsaka mwenzie ambaye alimkuta chini kabisa akiwa hajitambui na kumbeba Hadi juu.kisha alimuweka kwenye mtumbwi..alikua na jeraha dogo kichwani na damu zikichuruzika,alitega sikio lake na kusikiliza mapigo ya moyo na kuona angali anapumua na kuanza kumpiga piga kifua.
Mara ya kwanza ,mara ya pili na yatatu akafanikiwa kucheua maji yaliyomuingia..aliendelea na zoezi hilo huku pia akichota maji kwa kopo kuyatoa yalioanza kuingia kwenye mtumbwi.na ilimchukua takribani dakika 15 hadi yule mvuvi mwenzie fahamu zilimlejea,alishumshukuru Sana mungu,kisha kuendelea na zoezi la kutoa maji kwenye mtumbwi.baada ya kuyapunguza Sana ndio wazo la kurudi tena majini kuangalia kwenye lile boti iliowagonga kama kuna watu likamjia.
Alidumbukia tena kwa maji na kwa kasi aliogelea hadi ilipoangukia ile boti kubwa,alizama chini na kuangaika huku na huku kutafuta mtu lakini hakuona.na kurudi zake juu ya maji,akavuta hewa kidogo,kisha akaenda hadi ulipo mtumbwi wao,ambapo Sasa swahiba wake nguvu zilianza kumrejea,alimuambia aendelee na zoezi la kutoa maji ili yasiwe mengi mtumbwi ukazama kisha yeye alirudi tena kwenye lile boti kubwa.safari hii alizama na kuingia ndani ya boti kabisa.alikuta kijana mmoja wakizungu akiwa amebanwa na mtungi wa gesi kwenye viti vya boti hiyo kubwa.alifanikiwa kuondoa mtungi ule wa gas na kisha kuopoa mwili ule hadi ulipokua mtumbwi wao.wakati akitafakari afanye nini tena moja ya mashua ya wavuvi wenzie ilifika na kuwasaidia.

Wakiwa katika ile mashua ndio wale wavuvi wengine walitambua kijana yule wa kizungu bado angali anapumua..walianza utaratibu wakumpa huduma ya kwanza kwa kumpulizia hewa huku wakisukuma mapigo yake ya moyo.japo walifanikiwa kumtapisha maji zaidi ya mara tatu lakini hakuweza kupata fahamu hadi wanafika ng’ambo..walimkimbiza kwenye zahanati ya wilaya,sambamba na yule mvuvi mwenzie Kijazi ambaye alipata jeraha la kichwa.kisha walienda kwenye kituo Cha polisi mkuranga kutoa taarifa..
Haikua siku nzuri hata kidogo kwa kijazi aliwaacha wenzie wakirudi hospital kujua hali ya majeruhi wale,huku yeye akirejea nyumbani ambako alimkuta mama yake ameshaivisha ugali muda mrefu Sana,akimsubiri yeye arudi na kitoweo.alimuhadithia mama yeke mkasa mzima wa kilichotokea na wakashukuru mungu amerudi salama.walichemsha uji wakanywa na kulala.
Kesho yake alidamka alfajiri kama ilivyo ada yake na kuelekea ufukweni.hakua na chombo tena hivyo aliomba kujumuika katika vyombo vya watu wengine na kwenda baharini.
Walirejea na chombo mida ya Alasiri ambao walikuta kuna askari wakimsubiri.
"Wewe ndio kijazi"
NAAM ndio Mimi
"Sawa unahitajika kituoni,tunaomba utufuate"
Sawa afande ila ndio nimefika naomba angalau wasaa nipokea fungu langu
"Tupo hapa tangu asubuhi tunakusubiri wewe,watakutunzia wenzio,tunakuomba twende kwa hiari"
Hakua na jinsi tena..alimuomba kijana mmoja ambaye alikua rafiki wa marehemu baba yake amchukulie kitoweo chake na gawio lake la mauzo ampelekee mama yake.
Walifika kituoni na kukuta mkuu wa kituo akiwa wima anawasubiri.alipelekwa kwenye chumba maalumu Cha maelezo na kuhojiwa.chini ya usimamizi wa mkuu wa kituo.baada ya kutoa maelezo yake alichukuliwa na kupakiwa kwenye defender ya polisi na safari ya kuja Dar ikaanza.
Kwa muda wote huo kijazi hakuwa anaelewa kosa lake ni nini na kwanini yote haya yanatokea.na hata safari yenyewe ya kuja Dar hakuwa anaelewa ni wapi anapelekwa, kwani maisha yake yote hakuwahi kutoka nje ya mkuranga..
Yule kijana aliombwa kupeleka kitoweo kwa mama alifikisha na kumpa taarifa kamili mama mzazi,ambaye hakuweza kabisa kufanya lolote muda ule,haraka haraka Sana alielekea kituo kikuu cha polisi cha wilaya…hapakua mbali sana na nyumbani hivyo alifika wakati Kijazi akiwa kwenye mahojiano, alisubiri hadi polisi wamalize mahojiano yao ili naye azungumze na mwanae, lakini hakufanikiwa kupata hata dakika moja.kwani walipomaliza tu mahojiano alipakiwa kwenye defender na kusafirishwa.

Alilia Sana siku hiyo kuliko hata machozi aliyotoa kwenye msiba wa mumewe,alishuhudia mwanae anayemtegemea akipandishwa kwenye gari la polisi na kusafirishwa asipokujua,lakini kilichomuumiza zaidi kijazi bado alikua kijana mdogo wa miaka 16 na yeye hakua na uwezo wowote wa kumsaidia.

Alirudi nyumbani huku njia nzima akilia,na alishinda muda wote akilia mwenyewe ndani ya nyumba yao hiyo chakavu.alilia usiku kucha huku alimuomba mungu amlinde mwanae,na asubuhi palipokucha alirejea tena kituoni huku akilia kujua hatma ya mwanae.
Si mkuu wa kituo ama askari yoyote alikua na majibu kamili juu ya maendeleo ya kijazi ama kijazi anatuhumiwa kwa kosa gani. Zaidi zaidi walisisitiza tu yalikua ni maagizo toka makao makuu.
Wakati taharuki ikiwa inaongezeka kwa ndugu na jamaa wa kijazi,kwa kutojua nini na kipi ni kipi.
Madaktari na manenesi wa hospital ya wilaya Mkuranga walikua wakihaha kujua maendeleo ya yule kijana wa kizungu(majeruhi wa ajali).
usiku wa saa mbili na dakika 26 wa siku hiyo ya pili.watu sita walifika hospitalini wakiwa na magari mawili,moja toyota landcruiaer na nyingine toyota Van ambayo ilionekana vyema lilikua gari lakubeba wagonjwa,walimchukua yule kijana wa kizungu na kuondoka naye..

Siku iliofuata Mama kijazi kwa msaada wa majirani aliweza kwenda mjini kumuona mwanae,ambaye kwa muda wote huo hakujua ameshikiliwa kwa kosa lipi,na wala hawakua na ufahamu wowote juu ya Mambo ya sheria na taratibu zake,hivyo kila siku mama kijazi alishinda polisi central na kwamsaada wa vijana wavuvi wenzie na kijazi ndio aliweza pia kupata mahitaji yake ya kila siku..

Wiki mbili zilikatika Kijazi akiwa mahabusu,bila kusomewa shtaka lolote,hivyo iliamuliwa apelekwe kwenye gereza dogo la watoto watukutu pale upanga magharibi karibu hospital ya legency.
Huko ndio Kijazi alipokutana na Madam Aggie,mtaalamu wa saikolojia ambaye alikua akienda mara kwa mara kuwahudumia.kwakuwa gereza hilo pia ni sehemu ya mafunzo kwa watoto.ndipo uwezo mkubwa wa kuogelea wa Kijazi ulipoonekana..Mwanzo ilikua kama utani hivi mbele ya msimamizi wa gereza .
Ushauri wa Madam Aggie,wa kumruhusu kijazi akashiriki madhindano ya kuogelea yalikua yameandaliwa na mkuu wa majeshi Tanzania ulikua kama kioja flani.
Ila baada ya ushindi ule wa kwanza alioupata kwenye madhindano hayo msimamizi wa gereza alitoa kibali Cha kijazi kutoka kila jioni kwenda kwenye mazoezi ya kuogelea chini ya uangalizi wa Madam Aggie.
Na ikawa miezi sita imekatika hakiwa mahabusu kwenye kituo hicho,huku mama take mzazi alikwisha kata tamaa ya kumpata mwanae,na majirani pia walishachoka kujitolea hela za nauli za kwenda mjini kila siku.
Yalifanyika madhindano mengine ya michezo kwa taasisi za kijeshi Afrika Mashariki ambapo Kijazi alishiriki tena kushinda medani ya dhahabu.
Hapo ndio jicho la mkuu wa majeshi lilipomuona kijazi,na kuvutia na umahili wake wa kuogelea kwa kasi na pumzi aliyokua nayo.alipoambiwa ni mfungwa/mahabusu aliamua kulichukua faili lake ,ambalo Hadi wakati huo alikueleza haswa anashikiliwa kwa kosa lipi.

Chini ya usimamizi Madam Aggie aliruhusiwa kurudi nyumbani Mkuranga kumuona mama yake na kumuaga kwani alipewa nafasi ya kujiunga na jeshi la kujenga taifa ili kuendeleza kipaji chake cha uogeleaji.
Taarifa hizi zilirudisha tabasamu la bi Rehema mama Kijazi liliokosekana kwa miaka mingi Sana.Kijazi akajiunga na jeshi la JKT na madam Aggie alichukua jukumu la kumlea mama yake..
Miezi sita ya mwanzo ilikatika na kumaliza mafunzo kisha kwenda kwenye mashindano ya jumuiya ya madola Australia ambako alishinda medani ya shaba,aliporudi nchini akajiunga rasmi na jeshi la wanamaji.akiwa ni kijana wa miaka 18 kasoro,ujuzi wake uilimpa maisha katika mazingira yasiotarajiwa..

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

Love podcasts or audiobooks? Learn on the go with our new app.