DMX — MWANA HIP HOP ALIYEMJUA MUNGU ZAIDI

Earl Simon Almaarufu Kama Dmx,Msanii Nguri Wa Hip Hop Ambaye Amefariki Dunia Jana April Tisa,Akiwa Na Umri Wa Miaka 50.Kwa Taarifa Rasmi Ambazo Zimetolewa Na Familia Yake Jamaa Amepoteza Maisha Baada Ya Kusumbuliwa Na Tatizo La Moyo,lililosababishwa na Kiwango kikubwa Cha Matumizi Ya Madawa Ya Kulevya Cocaine.

Wakati Industry Ya Muziki Na Media Tanzania Na Dunia Nzima zikitangaza Kifo Cha Mwamba Huyo,Wengi Wa Vijana Wa Kizazi Cha Sasa Hawajapata Kufahamu Dmx Ni Nani Haswa.

Niseme Yapo Mengi Sana Yakumuelezea Nguri Huyu Wa Hip Hop,Aliyeweza Kuiokoa na kuisimamisha Hip Hop kwenye ramani na soko la muziki duniani Baada Ya Vifo Vya Tupac Na Notorius Big.

Dmx Ndio Msanii Wa Kwanza Wa Mziki Wa Hip Hop Duniani Aliyeweza Kutoa Album Tano Mfululizo Na Kufanikiwa Kushika Namba Moja Kwenye Chati Kubwa Zote Duniani Kama Billboard Nk

Wakati Kizazi Cha Leo Kikimuongelea Kanye West Na Album Yake Ya Injili Aliyofanya Mwaka Jana,Mwamba Dmx Alifanya Album Yake Ya Injili Mwaka 2011 Na Pia Kuhudumu Kama Mhubiri Huko New Jearsey ,Zaidi Ya Hilo Dark Man Katika Kila Album Yake Alioachia Huko Kulikua Na Nyimbo Moja Ya Gospel (Street Hiphop Gospel),Na Katika Moja Ya Vipindi Alivywahi Kuhojiwa Huko Nyuma,Mwenyewe Amekiri Kuwa Alikua Akiongea Na Mungu Wake Katika Kila Album Yake Na Zaidi Bibvlia Ndio Kitabu Chake Anachopenda Kusoma Kuliko Vyote.

Ameacha Album Tisa Zilitoka Official Chini Ya Usimamizi Wa Studio/Label Kubwa Alizosaini Lakini Pia Kuna Album 7 Zilizotoka Nje Ya Utaratibu,Mwamba Ameshiriki Katika Filamu 19 Hadi Anafariki Ila Wengi Wtu Tutamkumbuka Kwenye Movie Ya Romeo Must Die Iliotoka 2001 Akiwa Na Wakali Kama Jet Li Na Marehemu Aaliyah.

Kwamujibu Wa Mtandao Wa Youtube Zifuatazo Ni Nyimbo Zake Kubwa Tano Zilizofanya Vizuri Zaidi.

v Wimbo Wake Wa Slippin Ulitoka Mwaka 1998 Kwenye Album Yake Ya Kwanza Na Kupandishwa Youtube Mwaka 2011 ,Ndio Umeshika Namba Tano Ukiwa Umetizamwa Na Watu Milioni 54m

v Kutoka Kwenye Album Yake Ya Tatu Ya “The Grand Champ” Ilioachiwa Mwaka 2003,Nyimbo Ya Where The Hood At,Umeshika Namba 4 Ukiwa Umetizamwa Na Watu Milioni 84

v Namba Tatu Imekamatwa Na Singo Yake Ya Part Up Iliotoka Mwaka 2000 Ukiwa Imetizamwa Mara Milioni 118m

v Ruff Ryder Anthem Unasemwa Kama Wimbo Wake Mkubwa Kuliko Zote Katika Kipindi Chote Cha Muziki Wake,Ambao Aliuachia Rasmi 2001,Umetizamwa Mara Milioni 142..Wimbo Huu Ndio Uliomtoa Na Kumpa Utajiri,Mtayarishaji Maarufu Swizz Beats.

v X Gonna Give It To Ya ,Unapatikana Katika Album Yake Ya Tatu Ya Grand Champ Lakini Pia Ulitumika Kama Sound Truck Kwenye Movie Ya Romeo Must Die,Ndio Nyimbo Yake Iliotizamwa Mara Nyingi Zaidi Kwenye Mtandao Wa You Tube,Ukiwa Umetizamwa Mara Milioni 162

Dark Man X Ndio Kirefu Cha DMX ,Amekua Mtu Wa Matukio Ya Uhalifu Mara Kwa Mara Lakini Atakumbukwa Zaidi Baada Ya Kufungwa Mwaka 2001,Na Lipokuwa Gerezani Alisema Ameenda Kule Kwa Kusudi La Mungu La Mumpellekea Ujumbe Mfungwa Mmoja Ya Kwamba Mungu Anampenda Sana.Na Alipotoka Gerezani Aliachia Album Yake Ya The Great Depresion Yenye Nyimbo Nyingi Zenye Mahudhui Ya Dini.Kama Who We Web,Na Lod Give Me A Sign.

Rip Earl Simons.

--

--

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

Love podcasts or audiobooks? Learn on the go with our new app.

Get the Medium app

A button that says 'Download on the App Store', and if clicked it will lead you to the iOS App store
A button that says 'Get it on, Google Play', and if clicked it will lead you to the Google Play store