Alikaza macho yake na kunitazama kwa kina kama vile mtu akitazama kitu kwenye jua kali kabisa la saa sita. Kisha akaanza kukimbia, nilimfuata nyuma taratibu na bodaboda niliyemkodi tangu natoka nyumbani..

Alikatiza mitaa kwa kiasi kweli kweli,huku mara kwa mara akiangalia nyuma kutazama kama kuna mtu anamfutilia.nilipogundua hali ile nilimuomba yule bodaboda wangu apunguze mwendo zaidi ila awe makini kumfuatilia asitupotee kabisa.

Tulifanikiwa kumuhadaa na taratibu akawa anapunguza mwendo na mwisho kabisa akaacha kukimbia na kutembea kawaida.

Safari yake iliishia makaburini kwenye yale makaburi mawili tuliomkuta jana..alipanda juu yake akawa anaruka kutoka kaburi moja kwenda jingine..

Sikuweka papara ya kumfuata,kwakuwa alishaonesha hali ya kuniogopa nilipomuita jina lake,nilikaa robo saa nzima nikimfuatilia kwa makini anachofanya.hadi yule bodaboda alishindwa kunielewa

“kwani broo unamfahamu huyu kichaa” HAPANA

“sasa mbona unapoteza muda wako kumfatilia hivyo”

muda!!? Muda upi naupoteza hapa kijana?

“si huu unaotumia hapa,kama vip mimi nipe changu nikuache,upambane na hali yako.”

Tulia kijana hakuna haki yako utakayonyimwa. we subiri nimalize hili nitakulipa,na hivi nikukuomba unisaidie kumkamata huyu binti utanisaidia!?

“Mmmh! Mimi!? Hapana aiseee siwezi” KWANINI!? Alihoji Tena Liam

“nasikiaga vichaa wana nguvu sana,asije akaniua kama alivyomfanya mumewe”

Heee kumbe unaijua stori yake!?

“sasa nani asiyemjua Nia hapa kijijini!? Labda mgeni aliyekuja leo”

Na hivi ni kweli kabisa alimuua mumewe!?

Brazaaa kwa wanawake wa kijiji hiki,wala mimi sishangai ndio zao,labda tu uwe mume maskini au mzawa wa hapa”

ok sasa napata picha vizuri

“yaani braza hiki kijiji wengi wetu ni wakristo na wapenda dini lakini hawa dada zetu hili pepo la kuua sijui wamelitoa wapi!? Halafu sasa nikama wanafundishana ama sijui ndio fahari yao…ila nasikia huyu binti tatizo ni ukoo wa mume wake, hawakukubali kabisa kumuachia mali za mumewe wakamlisha yamini ndio akawa chizi fresh! Yaani kuna wakati akili zinarudi kabisa na unaongea nae fresh”

Binafsi niliona maongezi yake yamekua mengi,nikaanza kujisogeza kuelekea alipo Nia Nelson.

We unafanya nini hapo!?” nilianza kwa kumkaripia nione kama atashtuka ama kunikumbuka.lakini wapi ndio kwanza akakaa juu ya kaburi la mtoto na kunitazama usoni.nilisogea hadi alipo na kukaa kaburi la pili yake.

“wewe ni nani “ aliniuliza Nia

Mimi ni rafiki yako

“umeniletea chakula!?” hapana

“nguo zangu na mwanangu je!?” hapana

“sasa sisi tutavaa nini kwenda kanisani sikukuu ya leo!?” nilitafakari kidogo kisha nikamjibu

“nguo nimeziacha kulee wanapiga pasi ,twende ukachukue”

kweli eeeh twende mwaya

Tulishikana mikono nakuanza kutembea kuelekea ilipo bodaboda, nilimshikilia haswaa ili asiniponyoke maana pia alikua anatembea huku anarukaruka.

Ghafla tulipoikaribia pikipiki akaanza kupiga kelele

“niache niache niache nimesema niache,nasema siendi peke yangu” alijivuta kwanguvu toka mikononi mwangu ila kwakuwa nilishajiandaa kumbeba kwahali ile hakuweza kuchomoka,akaendelea kupiga kelele za kutaka nimuachie akamchukue mwanae lakini wapi sikumsikiliza,nilimvuta nakumbana kifuani kwangu kwa mikono yangu miwili.Na muda wote wapurukushani zile yule bodaboda na watu waliokuwa wakipita njia nao walipaza sauti zao wakinisii nimuache aende zake…

NUNUA EBOOK YA NYAKATI (Nia Nelson) KUSOMA MUENDELEZO WA STORI HII KWA LINK HII HAPA CHINI

https://www.getvalue.co/home/product_details/nyakati

--

--

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

Love podcasts or audiobooks? Learn on the go with our new app.

Get the Medium app

A button that says 'Download on the App Store', and if clicked it will lead you to the iOS App store
A button that says 'Get it on, Google Play', and if clicked it will lead you to the Google Play store