Alikaza macho yake na kunitazama kwa kina kama vile mtu akitazama kitu kwenye jua kali kabisa la saa sita. Kisha akaanza kukimbia, nilimfuata nyuma taratibu na bodaboda niliyemkodi tangu natoka nyumbani..

Alikatiza mitaa kwa kiasi kweli kweli,huku mara kwa mara akiangalia nyuma kutazama kama kuna mtu anamfutilia.nilipogundua hali ile nilimuomba yule bodaboda wangu apunguze mwendo zaidi ila awe makini kumfuatilia asitupotee kabisa.

Tulifanikiwa kumuhadaa na taratibu akawa anapunguza mwendo na mwisho kabisa akaacha kukimbia na kutembea kawaida.

Safari yake iliishia makaburini kwenye yale makaburi mawili tuliomkuta jana..alipanda juu yake akawa anaruka kutoka kaburi moja kwenda jingine..

Sikuweka papara ya kumfuata,kwakuwa…

“ Ubaya uanza pale nafsi inapohisi kuwa yenyewe ni yakipekee,inahitaji jicho la tatu,chuki na uadui uja pale nafsi yakipekee inapozidiwa au kushindwa..#turidhike na hali zetu #hatuazamtoano

DMX — MWANA HIP HOP ALIYEMJUA MUNGU ZAIDI

EARL SIMONS (DMX)

Earl Simon Almaarufu Kama Dmx,Msanii Nguri Wa Hip Hop Ambaye Amefariki Dunia Jana April Tisa,Akiwa Na Umri Wa Miaka 50.Kwa Taarifa Rasmi Ambazo Zimetolewa Na Familia Yake Jamaa Amepoteza Maisha Baada Ya Kusumbuliwa Na Tatizo La Moyo,lililosababishwa na Kiwango kikubwa Cha Matumizi Ya Madawa Ya Kulevya Cocaine.

Wakati Industry Ya Muziki Na Media Tanzania Na Dunia Nzima zikitangaza Kifo Cha Mwamba Huyo,Wengi Wa Vijana Wa Kizazi Cha Sasa Hawajapata Kufahamu Dmx Ni Nani Haswa.

Niseme Yapo Mengi Sana Yakumuelezea Nguri Huyu Wa Hip Hop,Aliyeweza Kuiokoa na kuisimamisha Hip Hop kwenye ramani na…

KWAHERI RAIS MAGUFULI “MIAKA SITA YA KISHUJAA SANA”

Maandiko yanasema kila nafsi itaonja umauti na sisi tu mavumbi na mavumbini tutarejea.hii inamaanisha ya kwamba hapa duniani si makazi ya nafsi zetu ya kudumu,tunapita tu na huu mwili ni mavumbi tu.

Usiku wa tarehe 17 March 2021 umekua mrefu zaidi kwa Watanzania kuliko usiku mwingine wowote ule tangu kuzaliwa kwa taifa hili.

Kwa Mara ya kwanza tumeondokewa na kiongozi mkuu wa nchi,jemedari na mzazi wa taifa anbaye bado hakuwa amemaliza muda wake.Rais John Pombe Joseph Magufuli ameaga duniani wakati akiwa bado ni Amri jeshi mkuu wa nchi.

Ni mengi Sana yapo…

NITARUDIA TENA NA LEO.

Mara ya kwanza kabisa hakuna aliyetaka kuamini Kama ni kweli inawezekana.japo mifano mingi ilitolewa lakini haikuwaingia akilini kabisa.

Mmoja wa maswahiba wa bwana yule akasema kamwe yeye hawezi kutoka kibali Cha kuruhusu ndugu yake anyanyasike,maana yeye aliona ile hali ni manyanyaso tu,aliona kuwa ni wzo kubwa Sana kwa ndugu yule kulitekeleza.alizidi kwenda mbali zaidi kwakumtaka ndugu yake huyo ambaye anamuona akinyanyasika kimawazo achague moja Kati mafungu mawili aliyoyatenga mezani.

Ila kwakuwa beans yule alikua na dhamira hiyo ya dhati naye hakutaka kuyumbishwa hata kidogo na jamii yake ile iliomzunguka.na hata alipotakwa achague fungu moja,bila kusita alichagua…

STORI YA KIJAZI.

Ni mzaliwa wa mkuranga,pwani.mtoto wa pekee wa bi rehema,marehemu baba yake mzee Hamis alikua mvuvi wa samaki katika bahari hindi.na ndio ujuzi pekee aliomrithisha mwanae kijazi.
Kijazi hakupata nafasi ya kuendelea na shule alipohitimu elimu yake ya msingi,sababu mama hakua na uwezo tu wakumnunulia sare za shule.
Hivyo akawa mara nyingi akijumuika na na wavuvi wengine kwenda kuvua na kisha kuwanadi samaki waliopata ufukweni na mara Chache Sana alizungusha Hadi mitaani.kwa ufupi yeye ndio alikua baba wa familia.
Alipenda Sana kuchezea maji,hivyo muda mwingi wa jioni utamkuta baharini akiogelea,mara Chache Sana ungemkuta yupo na wenzie,alipenda kuoga peke yake.
Na Hakua na…

HIVI NI KWELI !?

Ni swali jepesi lenye jibu la ndio au hapana,lakini kabla hujajibu linahitaji tafiti isiyo rasmi kujihakiki.

Iko hivi,bi mkubwa,mamaake mwenyewe yupo mjini baada ya kaziara kafupi ka kuwatembelea marafiki zake wa zamani miji kadhaa ya kusini mpaka kaskazini mwa Tanzania(kama mgombea vile 😂)
Wakati tumekaa tukipiga stori jinsi alivyoona mabadiliko ya nchi,maana kuna miji imepita miaka 20 tangu alipoenda mara ya mwisho.tbc wakawa wanaonyesha nyomi la kampeni za @tunduantiphaslissu akiwa mbarali
Nikamsikia akisema "NINGETAMANI APITE KASULU NIKIWA NIMERUDI,NAMI NIKAMUONE"
basi nami nikamjibu kimasikhara tu "tuombe uzima utamuona tu mama yangu,bado kuna miji mingi mnaweza kukutana huko"
Baada ya kumjibu hivyo…

TUJIKUMBUSHE

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo ni heri mama wee

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania, ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu hakika

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania, watu wengi wanakusifu,
Siasa yako na desturi, ilituletea uhuru
Hatuwezi kusahau sisi, mambo mema ya kwetu hakika

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania, Kaaribu wasio kwao,
Wenye shida na taabu, hukimbizwa na walowezi

Tanzania yawakaribisha, mpigane kiume chema wee

Tanzania Tanzania, heri yako kwa mataifa

Tanzania Tanzania, watu wako ni wema sana
Nchi nyingi zakuota, nuru yako hakuna tena
Na wageni wakukimbilia, ngome yako imara kweli wee

Tanzania Tanzania, Mola awe nawe daima

OPEN LETTER TO MY FELLOW

Mimi niko poa kabisa.Ila dunia haijaisha uchungu.na ingawa am lucky to have u on my side and my family too still dunia ni chungu kwangu.

Labda sijajua dhumuni langu katika hii dunia,ndio maana muumba akanipa wewe lakini nimeshindwa kujua ww ni nani !?
natafakari makasirikio ya hii dunia dhidi yangu,bado sijioni ni mkosefu wa kustahili hii adhabu.ni kweli sijui kosa langu,na wala sijui kwanini unataka unifunze adabu.
je ni kosa kuipenda dunia yangu!? je ni kosa kuiamini akili yangu !? ama kosa ni kukuweka pembeni yangu.!?

Naamini Mama & baba ni miungu ya pili ya…

SIO DHAMBI SIO UDHAIFU

Nilipokua mdogo Mlezi wangu aliniambia mara kwa mara mtoto wa kiume halii,hata pale niipoumizwa dhahiri aliniambia vumilia jikaze,wewe mtoto wa kiume..kiukweli maneno yale yalijenga msingi moyoni mwangu,nikawa mtu wa kutabasamu kila mara,kila siku.huzuni yangu haikuonekana machoni,nililia mwenyewe moyoni.kumbe nilijaza sumu ya ukatili na uchungu mwingi moyoni.nikawa muovu,muuaji na mzimisha furaha za wengi kwa tabasamu langu maana niliwafunza wengine pia kuvumilia hata pale kisu kilipokua shingoni mwao..
siku moja rafiki yangu mmoja alifukuzwa kazi wakati umebaki mwezi mmoja alipe kodi ya nyumba na kumalizia ada yake ya chuo. mshahara wake ulikua laki 6 na 80 akipiga na vi…

Dr.John Heshima

WRITER & STORYTELLER. ONLINE & PR MANAGER IR SPECIALIST

Get the Medium app

A button that says 'Download on the App Store', and if clicked it will lead you to the iOS App store
A button that says 'Get it on, Google Play', and if clicked it will lead you to the Google Play store